Mwanamke
aliyeasi dini nchini Sudan na kupata adhabu ya kifo amejifungua mtoto
mvulana akiwa jela mjini Khartoum kwa mujibu wa wakili wake.
Meriam Yehya
Ibrahim Ishag, aliolewa na mwanamume mkristo jambo lililopelekea
mwanamke huyo kuhukumiwa kifo mapema mwezi huu baada ya kukataa kusilimu
tena.
Ataruhusiwa kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu kutekelezwa.
Meriam aliyezaliwa na wazazi waisilamu, alihukumiwa na mahakama ya ya kiisilamu.
Bi Ibrahim alihukumiwa kifo kwa kosa la zinaa kwa sababu ameolewa na
mwanamume mkristo wa kutoka Sudan Kusini na kwamba ndoa yao haikubaliki
chini ya sheria ya kiisilamu ambayo inasema kuwa mwanamke muisilamu
hawezi kuolewa na mwanamume mkristo.
Kwa kosa hilo, jaji alimuhukumu adhabu ya mijeledi miamoja, adhabub
ambayo itatekelezwa pindi mama huyo atakapopata nafuu kutokana na
kujifungua.
Bi Ibrahim alilelewa kwa njia ya kikristo , dini ya mamake kwa sababu
babake aliyekuwa muisilamu hakuwepo katika maisha yake tangu utotoni.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International,
alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Zinaa mwezi Agosti mwaka 2013, na
mahakama ikamuongezea kosa la kuasi dini Februari 2014 aliposema kuwa
yeye ni mkristo wala sio muisilamu.
Sudan ina idadi kubwa ya waisilamu ambao wanafuata sheria za kiisilamu.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment