Hilo limedhihirishwa na John Waweru,
raia wa Kenya ambaye amefanikiwa kufuga kucha zake kwa muda wa miaka 12
na kufikia urefu wa futi moja na inchi 3.
Katika mahojiano yake na gazeti la Nairobi News, Waweru anaweka bayana kuwa kucha hizo ndizo zimekuwa chanzo kikuu cha kumwingizia kipato.
Anasema amefanikiwa kuzigeuza kucha hizo
kuwa mojawapo ya kivutio cha utalii nchini Kenya kutokana na kuwafanya
watalii kuzishangaa na hivyo kumpatia pesa kama malipo ya kivutio
hicho.
Ili kuzidi kuwavutia watalii Waweru amezipaka kucha zake rangi zilizopo katika bendera ya Kenya hali inayomwongezea mvuto zaidi.
“Nimezipaka rangi ya bendera yetu kwa
kuwa watalii wengi wanaokuja kupiga picha na mimi wanazipenda rangi hizo
ili kuwafurahisha wateja wangu,” anasema Waweru akiongea na Kenya News
Anasema siku biashara ikiwa nzuri ana uhakika wa kurudi nyumbani na Sh5,000 (sawa na Sh94,000 za Kitanzania).
Waweru (33) anasema tangu mwaka 2002
alipoanza kufuga kucha hizo hajawahi kuzikata wala kuzipunguza kutokana
na sababu yoyote ile.
“Baada ya kumaliza shule nilipata kazi
lakini kucha zikawa zinakua kwa kasi kiasi cha kunifanya nishindwe
kutimiza majukumu yangu nikaona bora niache kazi ili ziendelee kukua
bila kikwazo chochote, nazilinda sitaki zikatike kwa namna yoyote.”
Anafafanua kuwa kikubwa anachokifanya ni
kuilinda rasilimali hiyo akiamini kuwa ndiyo mtaji wake, hivyo siku
zote hujaribu kujiweka mbali na ugomvi au hatari yoyote itakayosababisha
kucha hizo kukatika.
“Tangu nimeanza kufuga kucha nimekuwa
mtulivu mno. Najiweka mbali na ugomvi ili nisije kupoteza chanzo changu
cha mapato. Nafahamu fika kuwa kupigana kunaweza kusababisha kucha zangu
zikatike kitu ambacho sitaki kitokee,” anasema.
“Hata pombe nimeacha kunywa. Najaribu
kufanya kila linalowezekana ili kucha zangu zisiingie kwenye hatari na
huwa nazifunika kuziepusha na purukushani.”
No comments:
Post a Comment