05 May 2014

HUU NDIO UKWELI: WASANII WA KIBONGO WANA HALI MBAYA SANA....!SOMA ZAIDI HAPA...

Kuna kilio kinasikika kwa mbaaali. Wanamuziki na wadau wanalalamika kuwa muziki wa Nigeria unapandishwa na Bongo Fleva inapotezewa. Cha kujiuliza ni iwapo muziki huu unabebwa au ni ubora wa kazi hizo ndio unaowavutia mashabiki.  
 
Madj wanajua ili watu wasiondoke katika “dancefloor’’ ni lazima wapige nyimbo za Nigeria. Bila kupiga Testmoney, Ayee, Skelewi, Away Dance, Ginger,  Mama Africa, Adama na nyingine usiku wa mpenda burudani hauwezi kuwa umekamilika.  
 
Ukweli ni kwamba hawa jamaa wameshaharibu fomesheni ndiyo maana sasa hivi wasanii wanabuni mbinu mbalimbali ili angalau waweze kupata kitu kidogo. Kuwakwepa na kutafuta njia nyingine siyo dawa, kinachotakiwa ni kuhakikisha Bongo Fleva inasimama na huu ugonjwa wa ‘Naija Muziki’  unatokomea katika mlango ulioingilia.  
 
Kuna tukio la hivi karibuni limetokea kwenye burudani ya Muziki. Mwanamuziki Davido alipotembelea nchini mwaka jana huenda alituibia kitu na sasa ndicho kinamfanya akombe mamilioni ya pesa.
Inawezekana Davido alipokuja alikusanya CD nyingi za kundi la Offside Trick kama siyo za AT na kwenda kutoka na wimbo mkali ambao sasa unafanya vizuri. Ukisikiliza wimbo wake, “Aye” una kila sababu ya kuamini kuwa Davido ameiba mahadhi ya mduara wetu na kwenda kufanya mambo mbele ya safari.  
 
Huu ndio ukweli
Bongo Fleva haipo dukani halikadhalika muziki wa Nigeria. Maana yake ni kwamba hakuna duka lolote sasa hivi linalouza cd za muziki. Nyimbo zote unazozisikia mitaani ni za kunyonya kutoka mtandaoni.  
 
Kuwezeshwa kwa mitandao kumeifanya dunia iwe kijiji. Leo hii huwezi kumdanganya mpenda burudani kuhusu wimbo mpya au sinema mpya iliyotoka. Ukifumba na kufumbua utakuta tayari anayo; iwe kwenye simu, kompyuta au cd. Kwa maana hii kumlaumu mtu fulani kuwa ndiye chanzo cha muziki huu kushika nchini hoja hii haitakuwa na ukweli wowote.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname