06 May 2014

HIVI NDIVYO TANKI LA MAFUTA LILIVYO LIPUKA JANA KATIKA BARABARA YA DODOMA MWANZA NAKUSABABISHA MAGARI KUKWAMA KWA MUDA


4

5

3

2

11
Msururu wa magari ukiwa mkubwa katika eneo hilo baada ya kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka.
7
Baadhi ya wananchi wakipiga picha wakati tanki la mafuta la kampuni ya B. Clarke Haulege Construction, Tanki hilo ni mali ya Bw. Bundala Kapela wa Igunga ni namba T634 BCZ lenye vyumba vinne na uwezo wa kubeba lita 40.000 za mafuta ya Petroli lililipuka majira ya Saa 11:00 katika barabara kuu ya Dodoma Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida wakati breki za tanki hilo upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto, Jambo lililomfanya dereva wa roli lenye namba za usajiri T 164 CGF aina ya Scania lililokuwa likivuta tanki hilo kusimamisha na kukata haraka tanki hilo huku akiondoa haraka injini ili kuepusha madhara zaidi ambayo yangeweza kutokea, Katika tukio hilo lililosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na msururu wa magari kushindwa kupita katika eneo hilo kutokana na moto mkubwa uliochanganyika na moshi kutishia usalama wa watumiaji wengine, hata hivyo baada ya moto kupungua kiasi askari wa usalama barabarani waliamuru magari yaanze kupitia pembeni mwa barabara hiyo ili kuendelea na safari hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.
 10
Wananchi na wasafiri mbalimbali wakitoka kuangalia tukio hilo.
 8
Askari wa usalama barabarani akihakikisha mambo yanakwenda sawana usalama unaimarishwa katika eneo hilo

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname