04 May 2014

HAPANA CHEZEA DIAMOND ... AIBUKA NA TUZO SABA KTMA 2014


Msanii wa kizazi kipya, Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz leo May 3, 2014 amedhihirisha kuwa yeye ni msanii mkali kwa kuchukua tuzo saba katika Tuzo za Kilimanjaro 2014 (KTMA).
Diamond amejinyakulia tuzo:
Msanii Bora wa Kiume,
Video Bora ya Mwaka.
Mtumbuizaji bora wa Muziki wa Kiume.
Wimbo Bora wa Afro Pop.
Wimbo Bora wa Mwaka.
Mtunzi Bora wa mwaka Kizazi Kipya.
Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana.

Hakika Diamond ameonyesha ukali wake, na kuonyesha kuwa yeye ni bora zaidi na anapendwa na watu.

1 comment:

  1. Inapendeza sana diamond anatoa changamoto kubwa sana kwa wanamuziki wengine hiyo itapelekea na wao pia watunge nyimbo nzuri na kutoa video nzuri ili kuleta ushindani. Na pia serikali itambue mchango wa wasanii katika jamii sheria kali zitungwe dhidi ya watu wanaohujumu kazi zao ili kuongeza maslahi yao mimi ni yangu hayo kwa leo nachukua tena fursa nyingine kukupongeza diamond kwa mafanikio uliyofikia ila pia iwe changamoto kwako USIBWETEKE punguza mambo mengine nje ya muziki ambayo yanaweza kukushusha kimuziki kuwa kioo bora kwa jamii inayokuzunguka. Nakutakia mafanikio mema wako shabiki toka Arusha KEEP IT UP.

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname