06 May 2014

DANGURO LA MAKAHABA LAFUNGWA NA SERIKALI...NI LILE LA MBAGALA

Hatimaye serikali imelibomoa eneo lililogeuzwa kuwa danguro la wazi, ambako vitendo vya ngono vilikuwa vinafanyika hadharani, Mbagala Zekhem, jijini Dar es Salaam.

Bomoa bomoa hiyo ilifanywa juzi na Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya gazeti hili kuandika habari ya kiuchunguzi ambayo ilibaini watu wa rika mbalimbali kujihusisha na biashara ya ngono ya wazi katika eneo hilo. Eneo hilo lililopo Mbagala Zakhem, limekuwa maarufu baada ya watu kuugeuza uwanja uliojengwa vibanda vya mbao kwa ajili ya biashara ya chakula, kuwa kama eneo huru la kufanyia vitendo vya ngono.

Katika kuonyesha kuwapo idadi kubwa ya wanaoshiriki kwenye biashara hiyo, kila sikuinaelezwa kukusanywa ndoo tatu ya mipira ya kiume (kondomu) iliyotumika.

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo, wameliambia NIPASHE Jumamosi kwamba bomoabomoa hiyo ilifanyika juzi saa 7:30 mchana kwa kutumia magari mawili aina ya kijiko huku polisi wakiweka ulinzi mkali.

"Kila mtu hakufahamu kama wangekuja hawa jamaa kubomoa sehemu hii, tuliona magari na polisi yakivamia na kuanza kubomoa," alisema Abdallah Saidi.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, alisema amekerwa na vitendo vya kinyama vinavyofanywa na watu hao, hivyo ameamua kupambana nao.

Alisema aliposikia kwamba kuna watu wanafanya ngono hadharani kwa makundi aliumia sana, kwani miongoni mwao wapo watoto. "Haingii akilini kuona watu wazima wanafanya mapenzi hadharani, ni jambo baya na linaharibu watoto wetu ni lazima kuchukua hatua kali," alisema.

Alisema tayari wamebaini kuwapo na madanguro mengine ya aina hiyo (hakuyajataja), kinachofanyika ni kuwa yanafuatiliwa kwa makini, kisha hatua zichukuliwe kuyatokomeza.

"Ukiachana na kukerwa kwangu, pia kwa sasa tupo kwenye zoezi la kusafisha jiji, hatutakubali kuona eneo la wazi linachafuliwa," alisema.INAENDELEA >>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname