15 March 2014

ANGALIA PICHA YA MWANAJESHI FEKI ANASWA AKIFANYA UHALIFU

Mohammed Musa Yusufu anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na sare feki za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

KIJANA mmoja aliyejulikana kwa jina la Mohammed Musa Yusufu maarufu kama Mwarami, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na sare pamoja na kutapeli watu kwa kuuza fomu feki za kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

“Mdogo wetu Omari alikuja nyumbani na kutuambia amekutana na mtu anayehusika na fomu za kujiunga na Polisi na kwamba zinauzwa kwa shilingi 250,000. Kwa kuwa hakuwa na hela, aliamua kuuza kitanda na godoro na fedha zingine akaongezewa na mama,” alisema mmoja wa dada wa kijana aliyetapeliwa, aliyejitambulisha kwa jina la Siwa. 
Alisema baada ya kupata kiasi hicho, Omari alimfuata mtu huyo akiwa na rafiki yake aitwaye Ali Kassimu ambaye naye alitaka kununua fomu hiyo. 
Baada ya kumpatia, walipewa fomu hizo na kuelezwa kuwa walitakiwa kusafiri kuelekea Tanga sehemu iitwayo Kibuku ambako ndiko ilipo kambi yao. SOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname