MSHINDI
wa Kombe la Dunia na gwiji wa Brazil, Rivaldo ameweka historia baada ya
kuonyesha picha akiwa na mwanawe uwanjani anayetumia jina la baba yaje
huyo.
Rivaldo,
mwenye umri wa miaka 41, aliingia uwanjani akitokea benchi wakati Mogi
Mirim wakitoa sare ya 1-1 na XV de Piracicaba katike mechi ya ligi ya
jimbo la Sao Paolo Uwanja wa Romildo Ferreira.
Ilikuwa mara ya kwanza anacheza sambamba na mwanawe huyo mwenye umri wa miaka 18, Rivaldo Junior.
Kinda Rivaldinho ana safari ndefu kama kweli anataka kufuata nyayo za baba yake, aliyejipatia umaarufu mkubwa kwenye soka.
Katika
mataji, Rivaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia maarufu kama
Ballon D'Or mwaka 1999 katikati ya miaka yake mitano ya kuichezea
Barcelona ambayo alishinda mataji ya UEFA Super Cup, mawili ya La Liga
na Kombe la Mfalme.
Aliiongoza
Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2002 kabla ya kwenda kuongeza taji
la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na vigogo wa Italia, AC Milan.
Busu tamu: Rivaldo akisherehekea Kombe la Dunia na shujaa mwenzake wa Brazil enzi hizo, Ronaldo.
Rivaldo,
ambaye pia amechezea Santa Cruz, Corinthians, Palmeiras, Deportivo La
Coruna, Cruzeiro, Olympiacos, AEK Athens, Bunyodkor, Sao Paulo,
Kabuscorp na Sao Caetano, alirejea kwa mara ya pili Mogi Mirim Desemba
mwaka jana ambako aliibukia kisoka. Pia ni rais wa klabu hiyo kwa sasa.
Rivaldo akifunga kwa mpira wa adhabu wakati Olympiacos ikifungwa na Liverpool katika mechi ya michuano ya Ulaya mwaka 2004
Rivaldo akifunga kwa tik tak Barcelona ikitoa sare ya 3-3 na Manchester United mwaka 1998
No comments:
Post a Comment