11 February 2014

MZEE KINGUNGE ATEMA CHECHE VITA YA DAWA ZA KLEVYA

* Adai bila kunaswa 'vigogo' ni kazi bure

* Asisitiza mfumo wa malezi, tamaa chanzo cha tatizo
Mzee Kingunge akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na blogu hii nyumbani kwake
WAKATI serikali ikitokwa povu la mdomo ikijigamba kuwa, itaongeza ukali dhidi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini, japo tatizo hilo linaloonekana kuzidi kuota mizizi, mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru ameibuka na kufichua sababu za biashara hiyo kushindwa kukomeshwa huku taifa likiendelea kushuhudia vijana ambao ni nguvu kazi ikiangamia kwa tamaa za utajiri wa watu wachache.
Mwanasiasa huyo amesema ni vigumu biashara hiyo kukoma nchini kama serikali na vyombo vyake vya dola havitawashughulikia na kuwakamata  'vigogo' wa biashara hiyo pamoja na kutengenezwa sheria kali itakayowafanya wahusika wajutie kujihusisha nayo na kuwatia woga watu wengine wanaoanza au kutamani kuifanya biashara hiyo.
Pia, amesema ni lazima serikali na jamii kwa ujumla ishirikiane katika kuwapa malezi na elimu bora watoto na vijana itakayowafanya wapende kufanya kazi na kujitegemea badala ya kuwa tegemezi, wavivu na wanaopenda anasa na tamaa ya kutamani vitu ambavyo hawana uwezo wa kuvipata.SOMA ZAIDI
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumb

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname