Akizungumza
na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka bungeni Dodoma, Mshenga ambaye
ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa chama hicho, alisema yeye
amechaguliwa baada ya kuonekana kwamba anazo sifa na vigezo vyote.
Alisema uamuzi uliochukuliwa na Mwenyekiti wa kumfukuza ni kuonesha wivu wa yeye kutochaguliwa kuingia katika Bunge la Katiba.
“Mimi
jina langu ndiyo lililopata bahati ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bunge
la Katiba, sasa sijui kosa langu lipo wapi? Huo ni wivu kwa sababu yeye
hakuchaguliwa licha ya kupeleka jina lake na mkewe,” alisema.
Aidha,
Mshenga alisema Mwenyekiti wa chama hicho, hana uwezo wa kumfukuza
uanachama, isipokuwa Mkutano Mkuu wa Chama wa Taifa. Hata hivyo, kauli
hiyo ya Mshenga ilipingwa vikali na Soud alipozungumza na waandishi wa
habari.
Soud
alieleza kuwa Mshenga amefukuzwa katika chama hicho baada ya kufanya
kosa la kugushi saini ya Naibu Katibu Mkuu wa chama katika majina
yaliyopelekwa Ikulu Zanzibar.
“Tunamfukuza
Mshenga, kwa sababu ametenda kosa la kugushi saini ya Naibu Katibu Mkuu
wa chama ili jina lake liingizwe katika mchakato wa majina ya chama
hicho,” alisema.
Alisema Mshenga kwa wadhifa wake, anaweza kufukuzwa uanachama na Mwenyekiti; na si Mkutano Mkuu wa chama hicho.
“Cheo
chake cha Mkurugenzi wa Sera na Mawasiliano anaweza kufukuzwa bila ya
kufanyika kwa Mkutano Mkuu...ni nafasi nne tu za viongozi ambao
kufukuzwa kwake lazima kupate baraka za Mkutano Mkuu,” alisema.
Soud
alikiri kuwa ni kweli alipeleka jina lake na mkewe, Farida Khamis Juma.
Alisema hakuna kosa, kwa sababu mkewe anazo sifa zote, ikiwemo ni
mwanachama halali, ambaye alikuwa miongoni mwa wanawake mstari wa mbele
waliokiunga mkono chama hicho.
Aidha,
aliilaumu Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar kwa kushindwa kufanya uchambuzi,
unaotokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jakaya Kikwete ambaye aliagiza wenyeviti wote wa vyama vya siasa, kupewa
kipaumbele katika mchakato wa Bunge la Katiba.
Alisema
ameshangazwa kuona kwamba yeye ndiye Mwenyekiti wa AFP Tanzania nzima,
lakini hakuteuliwa kuwa mwakilishi katika Bunge la Katiba.
CHANZO:HABARILEO
No comments:
Post a Comment