Kama ulifikiri bongo fleva ilianza
kulipa mamilioni miaka ya akina Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na
wengine, nikimaanisha kuanzia mwaka ya 2010, kwa leo inabidi ubadili
mawazo yako.
“Lakini uzuri wakati mimi naanza
kufanya, kazi zilifanyika na misingi za ile kazi zilikuwa zimekaa
tofauti na watu wanavyosikia. Kwa hiyo uoga hata wa mapromota ulikuwepo
wakati wanatusogelea. Kwa hiyo hatukuwa tunalipwa laki tatu viiile.”
Mbwana Mohammed aka MB Dog ameiambia tovuti ya Times Fm.
Huenda inawezekana ulikuwa hujui kwa
sababu wakongwe waliokuwa wanahit enzi hizo hawakuwa na tabia ya kuweka
wazi kiasi wanacholipwa kama wanavyofanya wakali wa bongo flava wa
kizazi hiki cha dijiti.
Mkali huyo wa ‘Latifa’ ameiambia tovuti
ya Times Fm kuwa alikuwa anakutana na milioni kadhaa kwenye show zake,
na kwamba kiasi kikubwa zaidi alichowahi kulipwa kilikuwa shilingi
milioni kumi nchini Burundi.
“Yaani mimi show ya kwanza nimeanza
kuifanya nimelipwa milioni tatu, show ya mwisho mimi kuifanya nimelipwa
milioni kumi...ambayo ndiyo ilikuwa show ya maajabu yaani...kwa ubongo
wangu nawaza naweza kufanya show tena ya watu wengi kama wale!! Nadhani
ilikuwa mwaka 2006.” Amesema MB Dog na kusisitiza, “milioni kumi za
kitanzania”.
Kumbe Bongo Flava ilianza kulipa zamani japo kwa wachache! Na huenda ni kwa sababu tu watu walikuwa hawaweki wazi wanachoingiza.
Hapa tumpigie picha Mr. Nice wa enzi hizo kwa kutumia mfano wa MB Dog.
Kama kweli mambo yalikuwa hivi, inaweza
kuwa moja kati ya sababu zilizozaa wazo kati ya wakongwe Juma Nature na
Lady Jay Dee kutaka Leo iwe ‘Kama Jana’
No comments:
Post a Comment