Jahazi lililokamatwa na madawa ya kulevya.
Zaidi
ya kilo 200 za madawa ya kulevya aina ya Heroin yamekamatwa na kikosi
cha polisi wanamaji katika Bahari ya Hindi yakisafirishwa kutokea nchini
Irani pamoja na mabaharia kumi na wawili kutoka nchi ya Irani na
Pakistani.
Kamanda wa
polisi kikosi cha wanamaji Mboje Kanga ameeleza kuwa tukio hilo
lililotokea usiku wa tarehe 4 majira ya saa sita usiku ambapo waliweza
kukamata jahazi hilo na mabaharia kumi na mbili wote wakiwa hawaijui
lugha ya Kiswahili wala Kingereza na jahazi lao halikuwa na utambulisho
wowote wa sheria za majini.
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti
dawa za kulevya, Godfrey Nzowa amesema jahazi hilo liliweza kukamatwa
baada ya kikosi cha polisi cha wanamaji kuendelea na operesheni zake za
doria majini na mara baada ya kulitilia shaka waliweza kulikamata na
baada ya kulikagua walikamata shehena hiyo ya madawa ya kulevya
aliyoyataja kuwa ni aina ya Heroin ambayo mengi huzalishwa nchini.
Chanzo: ITV
No comments:
Post a Comment