18 February 2014

ANGALIA PICHA YA MTOTO AOKOTWA AMEKATWA MAPANGA

Mtoto Ismail Barihegi.

MTOTO Ismail Barihegi, mwenye umri wa miaka 12 mkazi  wa Kijiji cha  Fukayosi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ameokotwa akiwa amekatwa  mapanga baada ya kudaiwa kuipeleka mifugo yao katika mashamba. 

Barihegi ambaye amelazwa katika Jengo la Mwaisela Wodi na 17, Muhimbili, alimwambia mwandishi wa habari hizi kwamba siku ya tukio (hakumbuki)alikuwa akichunga ng’ombe porini lakini ghafla walitokea watu  na kumwuliza kwa nini aliwaachia ng’ombe wake kufika shambani. Alisema aliwakatalia watu hao kwamba mifugo iliyokuwa shambani haikuwa ya kwao, na hata kuwaonesha ng’ombe wao, lakini watu hao hawakumwelewa.
“Walianza kunikata mapanga kichwani, begani na sehemu zingine za mwili, nililia sana huku nikiwaomba wanisamehe hawakunisikia.SOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname