26 February 2014

ANGALIA PICHA KIJANA AKAMATWA IKIIBA KANISANI

Emmanuel baada ya kupokea kichapo cha nguvu kutoka kwa wanachuo.
Kijana anayejulikana kwa jina moja la Emmanuel (30), amejikuta akipokea kipigo ‘hevi’ baada ya kukamatwa akiiba katika Chuo cha Theofilo Kisanji ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kanisani hapo, mchana kweupe ambapo jamaa huyo ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara kwa mara, alijikuta arobaini yake ikitimia na hivyo kutiwa mikononi mwa wanachuo ambao kabla ya kuhoji zaidi, walimshushia kipigo cha mbwa mwizi.

Wanachuo wakikagua baadhi ya vitu alivyokutwa navyo Emmanuel.
 “Huyu ndiye huwa anatuibia humu chuoni na kanisani, kila siku watu wanalalamika kuibiwa vitu vyao. Juzi tu, kuna watu waliibiwa simu, wengine fedha lakini hatukujua ni nani aliyekuwa akitufanyia hivyo, sasa huyu tutamkomesha,” alisema dada mmoja huku akiwa na furaha ya kukamatwa kwa jamaa huyo.

1 comment:

  1. Pole kibaka. ingia humu uangalie mtandao wa madawa ya kulevya. lol!!!!!!!!!!
    http://www.begorgeouswithjeddy.blogspot.com/2014/02/kufuru-ya-mtandao-wa-madawa-ya-kulevya.html

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname