Mwanasiasa wa Zambia bwana Frank Bwalya ameshtakiwa kwa kosa la kumfananisha rais wa nchi hiyo na kiazi. soma zaidi
Kutokana na mashtaka aliyofunguliwa akikutwa na hatia anaweza kufungwa jela kwa muda wa miaka mitano.
Siku ya Jumatatu akiwa kwenye radio mwanasiasa huyo wa upinzani alimtaja rais wa Zambia kama “chumbu mushololwa” ambapo alikuwa akimfananisha na kiazi.
Mwanasiasa huyo ambaye anatoka National Restoration Party (NRP) ameshafunguliwa mashataka na kesi itaanza kusikilizwa.
Mwaka 2005 kwenye nchi hiyohiyo ya Zambia mwanaume mmoja alifungwa jela miezi 9 kwa kumuabisha kwenye bar rais wa kipindi hicho Levy Mwanawasa.
Mwaka 2002 mhariri wa gazeti moja alikamatwa kwa kumuita Mr Mwanawasa “cabbage” na baadae mashtaka yalifutwa.
No comments:
Post a Comment