13 January 2014

MAJANGA....HATIMAYE PUB YA AUNT EZEKIEL YAFUNGWA GHAFLA

Aunt Ezekiel.
PUB iliyoibuka kwa muda mchache na kukamata ‘taito’ kubwa Bongo ya mwigizaji Aunt Ezekiel, Demonte imefungwa ghafla, haitoi huduma tena.Imedaiwa kuwa, pub hiyo iliyopo maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar, imefungwa kutokana na mhusika kushindwa kuiendesha.

“Imefungwa, nasikia gharama za vinywaji na wafanyakazi aliowaajiri zilikuwa juu akaona bora afunge,” alisema rafiki wa Aunt aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Paparazi wetu alishuhudia pub hiyo ikiwa imefungwa kwa zaidi ya miezi kadhaa, alipomtafuta Aunt, hakupatikana hadi tunakwenda mitamboni.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname