22 January 2014

LINAH AFUNGUKA KUHUSU SKENDO YA KUTOKA NA KIGOGO WA WIZARANI NA KUPACHIKWA MIMBA...!


STAA wa Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’ amepangua skendo inayomtafuna ya kutoka na kigogo mmoja wa wizara nyeti ya Serikali ya Tanzania na kupachikwa ujauzito.
Estelinah Sanga ‘Linah’.
Akizungumza na mwandishi wetu, Januari 17, mwaka huu, Linah alisema shutuma hizo zimemwandama wakati siyo za kweli na hana uhusiano wa kimapenzi na kigogo yeyote wa serikalini.
“Watu wamenizushia mambo kibao kuhusiana na ujauzito wakati sina na wala sijawahi kuwa kwenye uhusiano na kigogo yeyote wa serikalini, hata mtu anayetajwa sijawahi kumuona zaidi ya kumsikia tu. “Naomba nieleweke kuwa nina mchumba wangu na anajulikana hadi kwetu,” alisema Linah

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname