KITUKO CHA 2014: SAMAKI AINA YA SATO AONYESHA MAAJABU WILAYA YA BUNDA, AINGIA TUMBONI MWA MSICHANA WA MIAKA 12 KUPITIA SEHEMU ZA SIRI, DARUBINI ZA ASILI ZATHIBITISHA KUOONEKANA TUMBONI.
MAISHA ya mwanafunzi wa
kike mwenye umri wa miaka 12, (jina tunalihifadhi), anayesoma darasa la
tano Shule ya Msingi Bwanza, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, yako hatarini
baada ya kurukiwa na samaki aina ya sato, kuingia sehemu ya siri na
kukimbilia tumbani.
Tukio hilo limetokea
Januari mosi mwaka huu, saa 11 alfajiri,wakati mtoto huyo akichota maji
katika Ziwa Victoria ili aweze kumwagilia bustani ya nyanya, vitunguu
iliyopo kandokando
ya ziwa hilo.
Akizungumza na Majira,
kaka wa mtoto huyo (jina tunalihifadi), mwenye miaka 31, alisema tukio
hilo limewashangaza wakazi wa Kijiji cha Bwanza na vitongoji vyake.
Alisema mdogo wake
alikuwa akichota maji katika ziwa hilo akiwa amechuchumaa ndipo samaki
huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa wa nchi nne, aliruka kutoka majini,
kuingia sehemu yake ya siri na kukimbilia tumboni.
"Mdogo wangu alifanya
jitihada za kumvuta ili aweze kumtoa lakini alikimbilia tumboni na
kuanza kupata maumivu makali,kutokwa na damu nyingi baada ya kuparazwa
na miba ya
mgongo wa samaki huyo.
"Baada ya tukio hilo,
alirudi nyumbani kwa shida akijivuta na kuugulia maumivu...alimweleza
mama na ndugu zake juu ya mkasa huu, walimchunguza na kujaribu kuingiza
mkono sehemu za siri wakidhani watampata lakini hawakufanikiwa,"
alisema.
Aliongeza kuwa, baada
ya kumpeleka zahanati iliyopo kijijini hapo, hali yake ilizidi kuwa
mbaya akilalamika maumivu makali tumboni ambapo familia inaamini tukio
hili limetokana na imani za kishirikina hivyo waliamua kumtoa katika
zahanati hiyo.
"Tulimpeleka kwa mganga
wa kienyeji kijiji cha Amuyebe,wilayani Ukerewe...katika hali ya
kawaida samaki hawezi kumrukia mtu sehemu yake ya siri na kuzama
tumboni.
"Pamoja na kuchukua
uamuzi wa kumpeleka kwa mtaalamu,hali yake bado inazidi kuwa mbaya, hata
baba yetu alifariki katika mazingira yenye utata mwaka 2003," alisema.
Aliongeza kuwa, hata
kaka zake watatu na mtoto huyo nao walifariki kwa mfululizo mwaka 2004,
2005, 2006 ambao vifo vyao viligubikwa na utata mkubwa.
Mwenyekiti wa Kitongoji
cha Alwego anakoishi mtoto huyo, Bi. Reticia Bituro, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambalo limewashangaza watu na kuahidi uongozi wa
kitongoji hicho utaendelea kufanya uchunguzi zaidi.
Diwani wa Kata ya
Napindi, Bw. Elias Magoti ambaye yuko safari kuhudhuria kikao cha Baraza
la Madiwani Bunda Mjini,alikiri kupokea taarifa za tukio hilo kwa
mshangao mkubwa.
"Nitalifuatilia kwa
karibu baada ya kurudi kijijini kwa kufanya uchunguzi ili kubaini
kilichotokea kwani sijawahi kusikia tukio kama hili katika umri
nilionao," alisema.
Taarifa zilizopatikana
kutoka Ukerewe anakotibiwa mtoto huyo, zilisema kwa sasa hawezi
kuzungumza akizidi kulalamika maumivu makali ya tumbo na samaki huyo
bado hajatolewa. MAJIRA.
No comments:
Post a Comment