Ni
kosa ambalo limefanywa na wauza dawa au wasafirishaji wa hizo dawa
wenyewe manake mzigo ulianzia kusambaa kwenye duka la jamaa anaeuza
matunda kwa jumla kwenye mji hamburg ikiaminika ni baada ya kuwasili kwa
meli kutokea Colombia.
Wafanyakazi wa hizi supermarket ndio walitambua haya mabox ambayo ndani yake ndio kulikua na hizo kilo 140 za unga aina ya Cocaine saa kadhaa baada ya ndizi kuanza kuuzwa kwenye maduka yao.
Polisi wanasema kwa Ujerumani, wauza dawa za kulevya wana kawaida ya kutumia sana njia ya posta kusafirisha dawa za kulevya kwenye sehemu tofauti kuliko njia nyingine ambazo zimekua zikitumika.
Miaka minne iliyopita wafanyakazi kwenye supermarket nyingine waligundua dawa za kulevya zinazokaribia kilo themanini zilizokua zimefichwa kwenye maboxi ya ndizi, mzigo ulioingizwa Ujerumani kutokea Ecuador.
No comments:
Post a Comment