21 January 2014

Kijana mdogo aliyepigwa na Kanye West adaiwa kumuomba pesa ili yaishe kiaina.

Chanzo kimoja ambacho kiko karibu na kijana huyo, kimeiambia TMZ kuwa kijana huyo hataki kufuata njia za kisheria na kukimbizana mahakamani na kwamba mwanasheria wake amewaita watu wa Kanye na kuwaeleza nia ya kijana huyo kupewa mkwanja kiasi cha dola mia kadhaa ili yaishe.
Inawezekana kijana huyo anaogopa mkono wa sheria kwa kuwa Kim Kardashian alisema kuwa alimtolea maneno ya kibaguzi (n***er lover) yaliyoambatana na matusi.
TMZ imeripoti kuwa kijana huyo amekuwa haoneshi ushirikiano wa kutosha na polisi, na kwamba inasemekana licha ya kuwepo taarifa za kupigwa ngumi kadhaa hana majeraha.
Inasemekana pande hizo mbili sasa ziko katika makubaliano ya kuyamaliza kinyumbani na kuachana na njia ya kushitakiana.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname