Kwa muda mrefu kumekuwepo na taarifa
za ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu;
tumesikia walemavu wa ngozi (Albino)
kwa namna walivyofanyiwa na wanavyoendelea kufanyiwa ukatili kisa eti Imani za
kishirikina.
Pamoja na yote uliyosikia lakini
hebu fuatilia kisa hiki, ambapo mlemavu asiyejiweza kabisa anavamiwa, anabakwa,
anapewa Mimba, mwisho wa siku
anajifungua, lakini baada miaka
kadhaa mwanaye aliyemzaa akiwa mzima
naye ghafla anakuwa mlemavu –
Tangu nchi yetu ipate Uhuru waka
1961 Serikali kupitia Idara ya Ustawi
wa Jamii imekuwa inatoa huduma kwa
watu wenye ulemavu
bila kuwa na sera timilifu.
Kuwapo kwa Sera ya Taifa ya
Maendeleo na Huduma kwa Watu
wenye Ulemavu ni matokeo ya miaka
mingi ya majadiliano
baina ya Serikali na wadau. Pamoja
na kutokuwapo kwa sera,
Tanzania imekuwa inajihusisha na
mipango mbalimbali ya Kitaifa na
Kimataifa inayohusu masuala ya
ulemavu.
Kimataifa Tanzania imesaini mikataba
mbalimbali kuhusu
watu wenye ulemavu hususan mikataba
ya Haki kwa watu wenye
Ulemavu (1975), Haki za Mtoto (1989)
na Haki na Fursa sawa kwa Watu wenye Ulemavu (1993).
Barani Afrika, Tanzania ni miongoni
mwa nchi waasisi wa Mpango wa
utekelezaji wa muongo wa Watu wenye
Ulemavu na mwanachama
wa Taasisi ya Marekebisho kwa Watu
wenye Ulemavu
(African Rehabilitation Institute –
ARI).
Hapa nchini serikali imechukua hatua
kadhaa ikiwa ni pamoja na
kampeni za chanjo ya kuzuia ulemavu
utotoni (kwa mfano polio), kutunga
sheria zinazolinda maslahi na kuboresha maisha
ya watu wenye ulemavu
kuwapo kwa swali kuhusu ulemavu
katika sensa ya Taifa ya watu na
makazi (2002) na ile ya mwaka jana
(2012) na mandalizi ya kuridhia
mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu
Haki na Fursa Sawa kwa Watu wenye Ulemavu.
Sera inatoa mwongozo na inaweka
vigezo vya utoaji huduma.
Sera imejengwa kwa kuzingatia
utamaduni wetu na inalenga katika kuleta
maendeleo, haki na heshima kwa Watanzania
wenye ulemavu.
Changamoto iliyopo ni kutafsiri kwa
vitendo matumaini yaliyomo
kwenye Sera hiyo na kilichopo tu ni
kwamba kundi hili limekuwa
likikumbukwa pale tu linapotokea
janga au unyanyasaji fulani na
baada ya hapo hakuna tena
atakayejali na kulitilia maanani,kwani
kukosa kwao huduma mbalimbali za
jamii, kunawafanya walemavu
waathirike kisaikolojia na wengi wao
kukata tamaa ya maisha.
Pamoja na jitihada hizo za serikali
lakini bado kuna ukweli usiopingika
kwamba kuna baadhi ya walemavu ambao
serikali haijawafikia mahali walipo,
lakini kibaya zaidi hata jamii
yenyewe inayowazunguka haijaona umuhimu wa
kuwatolea taarifa mahali husika.
Miongoni mwa watu wenye ulemavu
ambaye anaonekana wazi kwamba
yuko katika hali ngumu huku serikali
ikiwa haijui taarifa zake lakini
kibaya zaidi jamii nayo ikionekana
kumtenga na kutomjali ni
Mwanamke Mary Petro (51) mkazi wa
kitongoji cha Sima kijiji na
kata ya Bupandwa wilayani Sengerema
Mkoani Mwanza.
Mlemavu huyo ambaye hana uwezo wa
kutembea,huku akiwa ni mtu
mwenye kubebwa na watu wawili wakati
wowote anapotaka kufanya
jambo lolote ikiwa ni pamoja na
kwenda kujisaidia haja kubwa ama
ndogo,kula chakula mwenyewe kwa
kutumia mikono yake miwili hilo ni jambo ambalo halijawahi kumtokea tangu
azaliwe miaka 51 iliyopita.
Mary ambaye hana uwezo wa kutembea
kutokana na miguu yake
kulemaa ambapo alizaliwa akiwa na
hali hiyo, mikono yake ikiwa
imekunjamana huku ikiwa imelalia
kifuani mwake, hawezi kulala kifudifudi,
wala ubavu yeye ni mtu wa kulala chali na
anapowekwa ni hapo hapo hadi atakapokuja kuondolewa ama kusogezwa kutoka sehemu
moja kwenda nyingine.
Hakika maisha anayoishi Mary ni
magumu huku akikabiliwa na changamoto
ya kukosa ulinzi wamaisha yake mara
kwa mara,hali inayopelekea wakati
mwingine kushinda njaa kwa kukosa
chakula kutokana na waangalizi wake
kuwa shuleni ama kwenda kwenye
mahemezi!.
Ugumu wa maisha ya Mary yamekuja
kutokana na wazazi wake
wote wawili (Baba na Mama) ambao
anawaelezea kuwa walikuwa
walinzi na msaada wake wa karibu
katika maisha yake tangu alipozaliwa kufariki Dunia.SOMA ZAIDI HAPA
No comments:
Post a Comment