Mchezaji wa zamani wa klabu ya soka ya Aston Villa, Thomas Hitzlsperger amejitangaza kuwa ni shoga.
Mchezaji huyo mwenye miaka 31 aliyeshinda vikombe 52 na Ujerumani na
aliyewahi kuzichezea pia West Ham na Everton, aliweka hadharani habari
hiyo kwenye gazeti la Die Zeit. Hitzlsperger anakuwa mchezaji maarufu
zaidi duniani kujitangaza hadharani kuwa ni shoga na amesema huu ni muda
mzuri kufanya hivyo.
Kiungo hiyo aliyestaafu soka mwezi September mwaka jana amesema
aligundua katika miaka michache iliyopita kuwa angependa kuishi pamoja
na mwanaume na kuongeza kuwa: Sijawahi kujionea aibu kwa jinsi nilivyo.”
No comments:
Post a Comment