Mshindi wa taji la urembo wa Venezuela
mwaka 2004 (Miss Venezuela 2004) Monica Spear ameuawa kwa kupigwa risasi
na majambazi jumatatu, January 6.
Kwa mujibu wa The Associated Press,
Majambazi hao pia walimuua kwa risasi mumewe Henry Thomas Berry
aliyekuwa naye kwenye gari, na kumjeruhi mguuni mtoto wao wa kike mwenye
umri wa miaka 5 anayefahamika kwa jina la Maya.
Ripoti zilizotolewa na maafisa usalama
wa Venezuela zinadai kuwa Monica ambaye pia ni muigizaji maarufu wa
tamthilia (Soup-Opera), alikuwa na mumewe na mwanae huyo wakitoka
mapumzikoni na kurudi Caracas, lakini bahati mbaya gari lao lilipata
pancha hivyo wakalazimika kupaki pembeni ya barabara.
Majambazi walitumia nafasi hiyo
kuwavamia, lakini Monica na mumewe walijifungia kwenye gari na kufunga
milango ya gari wakiwa na mtoto wao ili kujinusuru.
Majambazi hao walianza kufyatua risasi.
Director wa upelelezi wa Polisi wa Venezuela, Jose Gregorio amesema
takribani risasi sita zilifyatuliwa na majambazi hao, na kwamba mtoto
Maya anaendelea vizuri na matibabu.
Monica Spear aliwahi kuzing’arisha tamthilia nyingi ikiwa ni pamoja na tamthilia maarufu ya ‘Pasion Prohibida’.
No comments:
Post a Comment