KATIKA Hali ya isiyo kuwa ya kawaida, Bilionea wa Hong Kong
ametangaza dau la zaidi ya Paundi 40 milioni kwa mwanaume yeyote
anayeweza kumuoa binti yake msagaji.
Mfanyabiashara huyo wa meli za biashara na mizigo na
muendelezaji majengo Cecil Chao Sze –Tsung anaonekana kuchoshwa na
mahusiano ya binti yake Kiki kwa binti mwingine wa kike kwa karibu miaka
tisa.
Mfanyabiashara huyo wa Hong kong alikuwa na nia ya kumrithisha
himaya yake binti yake huyo lakini kwa masharti ya kuolewa katika
desturi za kistaarabu na siyo kuwa na mahusiano na mwanamke mwenzake.
Taarifa zinasema kwamba kwa kuangalia ukubwa biashara yake na
amewapa baadhi ya makampuni zake wanawe wengine wawili na fedha za
kutosha, lakini tajiri huyo Chao anataka wanawe wawe na maadili mema
katika jamii na sitabia za ovyo.
Chao mwenye umri wa miaka 77 aliliambia gazeti la Malaysia
Nanyang Siang Pau kwamba angeweza kutoa fedha mara mbili ya hizo katika
kuvutia wanaume wengi kujitokeza kwa ajili ya kumuoa mwanae.
Binti huyo anaonekana kama amechanganyikiwa kwa uamuzi wa baba
yake kumpa masharti ya kuolewa kabla ya kurithi mali na fedha taslimu za
baba yake.
Amesema kwamba fedha si kitu cha kumvutia mwanaume au yeye kumpenda mwanaume kwa sababu ya kupenda ni utashi wa mtu binafsi.
“Napenda kuwa na furaha kufanya urafiki na mtu yeyote tayari
kuchangia kiasi kikubwa cha fedha kwa jamii na upendo wangu ni kwa watu
wote na si kwa sababu ya fedha za baba yangu,” amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya maendeleo ya Cheuk Nang,
ambaye pia ni mwanaharakati wa LGBT anasema kwamba kwa kipindi kirefu
watu wamekuwa wakikiuka haki za mashoga na ndiyo sababu ya kushirikiana
karibu na Big Love Alliance ambacho ni kikundi cha kutetea haki za
mashoga Hong Kong na kutaka haki za mashoga kuwa sheria na kupitishwa na
serikali.
CHANZO-MOBLOG
No comments:
Post a Comment