Habari zilizopatikana kutoka kwa
mashuhuda na baadaye kuthibitishwa na gazeti hili, zilisema Ferooz
alikuwa akivuta bangi katika eneo hilo kabla ya majirani wanaokerwa na
tabia hiyo, kupiga simu polisi wakitaka kukomeshwa kwa jambo hilo.
“Hapana tumechoka na tabia zao, kila
ukipita hapa unakula ‘marashi’ ya bangi tu, vilevile sisi tuna vijana
wa rika lao, hawa vijana wanaopita hapa wanasoma, tunaogopa sana
wasije wakajiunga na wao hapa kula ganja,” alisema mama mmoja ambaye
hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Ferooz akiwa amepigwa pingu na mwenzake.
Ilidaiwa kuwa msanii huyo pamoja na
wenzake wamekuwa na kawaida ya kukaa katika kijiwe hicho kila siku na
kuvuta bangi huku baadhi yao wakitumia madawa ya kulevya.
Baada ya kutiwa nguvuni kwa vijana hao,
wakazi wa maeneo hayo wamewamwagia sifa Mkuu wa Kituo cha Polisi
Mabatini aliyefahamika kwa jina moja la Mapunda kwa jinsi
alivyofanikisha askari kuwahi eneo hilo la tukio.
...Akishushwa kutoka kwenye gari.
“Tulipopiga simu polisi, hatukutegemea
kama ingekuwa haraka hivyo, tunashangaa baada ya muda mfupi, wakaja
eneo hili, kwa kweli huyu mkuu ni mfano wa kuigwa, maana siku hizi
likitokea tukio lolote lile ni dakika chache gari limefika,” alisema
mkazi mmoja wa eneo hilo.
Ferooz, mkali wa kibao cha Starehe baada
ya kufikishwa kituoni hapo alichukuliwa maelezo yake kabla ya kuwekwa
rumande. Hadi gazeti hili likienda mitamboni haikufahamika siku ya
kufikishwa mahakamani kwa wahalifu hao.
No comments:
Post a Comment