28 January 2014

ETI HIZI NDO GHARAMA ZA KUOA IFIKAPO MWAKA 2017



Ikifika mwaka 2017 na bado hujaoa basi ujue

Possibility ya wewe kuoa ni ndogo sana.Sio kwa

sababu wanawake watakuwa wameisha,LA hasha!

Ila hutaweza ku-afford kuoa labda umtoroshee

msichana wa watu Gheto kwako uishi nae

kinyumba ,ilakuoa jasho la meno litakutoka.

Ukipeleka Ombi la kuoa ujiandae kwa gharama

zifuatazo kutoka Familia ya Bibi Harusi Mtarajiwa:

1.Blanketi la Bibi kutoka Home Shopping centre

vipisi viwili,rangi ya Purple

2.Blackberry Q10 ya Mshenga

3.iPhone7 Water Proof(itakuwa imetoka) ya Baba

Mkwe

4.3-Piece-Suit ya NGOWI. kwa ajili ya Mjomba wa

Bibi harusi aliyemsomesha Bi harusi sekondari

huko mwanalugali

5.Samsung Galaxy 9 Bold-Wipe Screen ya Mama

wa Ubatizo wa bibi harusi

6.iPad ya Kungwi wa bi harusi

7.Koti la Single button Leather by Martin Survivor

Kadinda kwa babu wa bi harusi kutoka Ileje

8.Mahari itajumuisha Less-Wig Brazillian Hair kwa

mama mzaa chema,na Table sets za mninga kutoka

Orcadeco..Hapo bado hujanunua Suti yako,Shela

ya Bi Harusi ambaye atang’ang’ania litoke

Uturuki,na hapo ana kijacho chako cha miezi 4

kishaanza kutuna kama kitenesi,bado hujalipia

Ukumbi Mwika Social Hall,hujammalizia MC

Luvanda milioni 4 ya kuwa MC wa harusi

yako…THUBUTUU YAKO!

Ukipewa Bili TOTAL utakuwa umehamishia mawazo

kumalizia ujenzi wako wa nyumba iliyoko Site kule

Goba,utaona kuoa ni upotevu wa hela na muda.

Ndugu yangu heri uoe sasa,usiwaone watu

wamechangamka kuoa hii miaka 2 ukajua ni bahati

mbaya,WAMEONA MBALI..Ikifika 2017 utaomba

Poo,sasa hivi we jishaue kuchagua-chagua tu Mke

wa kuoa kama uko mitumbani Karume,Heri uoe

huyohuyo hata kama miguu yake imepinda kama

Upinde wa Mvua itanyooka mkiwa Honeymoon….

n mtazamoooo

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname