Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe
Beach,
Dar, Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Sepetu imetolewa hukumu
yake baada ya Wema kuomba iharakishwe kwakuwa alikuwa anasafari.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Global Publishers, Wema sepetu amehukumiwa kifungo
cha miezi mitatu gerezani ama faini ya shilingi laki moja kwa maana ya
elfu hamsini kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa
hayo mawili ya kupiga na kutukana.
Baada
ya kusomewa hukumu hiyo wema alitoa laki moja hiyo iliyokuwa
ikihitajiwa na mahakama kabla ya kuachiwa huru kuendelea na mishe zake
nyingine
No comments:
Post a Comment