23 December 2013

"SITAKI MALUMBANO NA DIAMOND"...DAYNA AFUNGUKA..SOMA ZAIDI HAPA.


Mwanaisha Said Nyange ‘Dayna’.
MWANADADA anayetamba na kibao cha Mimi na Wewe, Mwanaisha Said Nyange ‘Dayna’ amefunguka kuwa hataki kabisa kumzungumzia msanii mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Dayna aliyasema hayo hivi karibuni alipoulizwa kuhusiana na bifu lake na Diamond lililotokana na kumwibia wimbo wake ambapo alisema hataki kumzungumzia kabisa Diamond kwa sababu hataki malumbano kwani hivi karibuni amezungumza maneno mbofumbofu kwenye vyombo vya habari.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Mimi sitaki malumbano na Diamond  kwa sababu amekuwa akizungumza mengi sana kwenye vyombo vya habari mengine ya kuniponda na mengine ya kawaida hivyo sitaki malumbano kabisa mimi niko kikazi zaidi yeye aendelee tu”, alisema Dayna. -GPL

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname