AFRIKA Kusini inamtafuta mkalimani feki wa kutumia ishara za viziwi ambaye alishindwa kufasiri walichokisema viongozi mbalimbali kutoka duniani wakati wa ibada ya kumkumbuka aliyekuwa rais wa nchi hiyo Nelson Mandela iliyofanyika Jumanne wiki hii.
Mtu huyo asiyefahamika na aliyekuwa na pasi zilizotolewa kwa ajili ya usalama eneo hilo, alikuwa amesimama karibu na viongozi hao wakati wanahutubia katika uwanja wa Soccer City wenye uwezo wa kuingiza watu 95,000 ambapo jamaa huyo alionekana akifasiri lugha mbalimbali kimakosa.
“Ulikuwa ni upuuzi mtupu, hakupatia chochote na alishindwa hata kutoa alama ya kusema ‘asante’,” alisema Delphin Hlungwane, mkalimani wa ishara wa chama cha viziwi cha Afrika Kusini ( DeafSA) ambacho kimelaani tukio hilo.
Pamoja na kwamba serikali ya nchi hiyo ilikuwa msimamizi wa sherehe hiyo, lakini jamaa huyo asiyefahamika mwaka jana alifanya hivyohivyo kwenye mkutano wa chama cha African National Congress cha nchini humo ambapo Rais Jacob Zuma alikuwa anahutubia.
No comments:
Post a Comment