26 December 2013

NOUMA...MONALISA, MAMA’KE WAFUNIKA NGOMA YA KIZARAMO KWENYE "SHUGHULI"...TAZAMA PICHA HAPA..

MWIGIZAJI Yvonne Cherry ‘Monalisa’ na mama yake, Suzan Lewis ‘Natasha’ wamewaacha watu midomo wazi baada ya kuonesha uhodari wa kucheza ngoma ya kizaramo.
Natasha na Monalisa wakicheza ngoma.
Mastaa hao walionesha utundu huo juzikati walipokuwa katika hafla ya mahari ya msanii mwenzao, Vanita Omary ambapo mwanamuziki Siza na kundi lake walipoimba nyimbo hizo, alianza kuinuka Monalisa kisha mama yake na kuanza kucheza kwa ustadi.
Monalisa na mama yake wakicheza ngoma za Kizaramo na wageni waalikwa.
“Sikujua kama akina Mona ni wazaramo na wanajua kuicheza ngoma yao, ukweli nimewakubali wamekumbuka kabisa asili yao leo ni balaa,” alisema mama Hawa, mmoja wa waalikwa.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname