MAYOWE,makofi na miluzi vimetawala nje ya Uwanja Mdogo wa Ndege wa Arusha (Arusha Airport) mara baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia aina ya Boeing 767, kufanikiwa kuruka kwa usalama kiwanjani hapo.
Ndege hiyo ilitoa kwa makosa (kama taarifa ya TCAA ni sahihi) uwanja mdogo wa Arusha Desemba 18 mwaka huu, majira ya saa sita mchana.
Ndege hiyo ilianza kuwasha injini zake saa 11:40 na ilipofika saa 11:47 asubuhi iliruka juu hata kabla hajamaliza njia ya kukimbilia ya uwanja huo.
Baadhi ya mashuhuda waliofurika pembeni mwa uwanja huo kabla ya ndege kuruka,kushuhudia ndege hiyo ni pamoja na raia wa kigeni, aliyejitambulisha kwa jina la Peter Swan, aliyesema ameacha kazi zote
ili aone bahati nasibu ya ndege hiyo kuruka, kwa sababu ni kubwa na uwanja mdogo.
Naye Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege Vidogo Tanzania, Thomas Haule, alisema anamshukuru mungu ndege hiyo kuweza kuruka salama na tayari ilipofika saa 6:05 mchana ndege hiyo iliweza kutua Uwanja wa
Kimataifa (KIA) salama salimini.BOFYA HAPA KUANGALIA VIDEO NAMNA NDEGE HIYO ILIVYOPAA
Alisema pamoja ndege hiyo kuwa na uzito wa tani 300, iliweza kuondoka bila kuacha athari katika, hivyo inaonyesha miundo mbinu ya uwanja huo ni mizuri.
No comments:
Post a Comment