Geez Mabovu mtoto wa Doll South yuko katika hali mbaya
kiafya na amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kuzidiwa
ghafla wakati akisubiri kufanya show mjini humo akiwa na Jan B na Songa.
Songa ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuwaopa taarifa fans wa Mabovu na kuwaomba waendelee kumuombea.
“ASANTENI SANA IRINGA,SIKUTEGEMEA MNAPENDA HIP HOP KIASI
KILE...MLITISHA SANA. ILA KUNA HABARI MBAYA NDUGU YETU GEEZ MABOVU HALI
YAKE SIO NZURI AMELAZWA,NAOMBA TUMUOMBEE ARUDI KATIKA HALI YAKE YA
KAWAIDA. ASANTENI”
Songa ameueleza mtandao wa Bongo5 kuwa Mabovu alizidiwa ghafla kabla ya show na akapelekwa hospitali ya mkoa.
Mapema jana ,Geez Mabovu aliongea na tovuti ya Times Fm na kueleza
kuwa alienda nyumbani kwao Iringa ambapo alikuwa hajaenda kwa muda mrefu
na kwamba alienda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa (December 25) na
familia yake.
Rapper huyo aliongeza kuwa ameamua kuacha kutumia pombe kuanzia
January Mosi mwakani kutokana na kutaka kufanya mabadiliko zaidi katika
maisha yake.
Tumuombee Geez Mabovu apate nafuu na apone haraka.
No comments:
Post a Comment