25 December 2013

Milovan akubali kuifundisha Yanga..SOMA ZAIDI HAPA...!

KOCHA wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic amesema yuko tayari kuinoa Yanga kama watamuita achukue nafasi ya Ernie Brandts.

Yanga iko katika mchakato wa kusaka kocha mpya baada ya kumfuta kazi Brandts baada ya kikosi chake kulala kwa mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe.

Akizungumza moja kwa moja kutoka Cacak, Serbia, Milovan alisema hajapata ofa yoyote kutoka Yanga lakini ikitokea hivyo kama kocha anayefuata weledi, mara moja atachangamkia ofa. 

“Kama Yanga wakisema, basi mara moja nitachangamkia ofa. Ukocha ndiyo kazi yangu na niko tayari kuja kama itatokea hivyo.
“Ukiangalia kikosi cha Yanga sasa kina wachezaji wangu wa zamani watano, hivyo nusu ya timu nimeishawahi kufanya nao kazi, maana yake kazi haitakuwa ngumu sana,” alisema Milovan.

Milovan aliwataja wachezaji watano walio Yanga ambao aliwahi kufanya nao kazi kuwa ni Juma Kaseja, Ally Mustapha ‘Barthez’, Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa na Emmanuel Okwi.
Tayari Yanga iko kwenye mkakati wa kusaka kocha mpya kuchukua nafasi ya Mholanzi huyo ambaye sasa ameishakabidhiwa barua ya kufutwa kazi. 

Milovan ni moja kati ya makocha wenye heshima kubwa kwenye soka la Tanzania baada ya kuiongoza Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara huku ikionyesha kiwango cha hali ya juu.

Lakini kocha huyo ana rekodi nyingine baada ya kuiongoza Simba kuichapa Yanga mabao 5-0 kwenye Ligi Kuu mwaka juzi.
Kama atafanikiwa kupata nafasi ya kuinoa timu hiyo ya Jangwani inaaminika kuwa itakuwa moto wa kuotea mbali huku ikipiga pasi za uhakika

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname