Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred hajui Kiswahili? Well, tuliowahi kukaa naye kidogo tunaweza
kumtetea
kuwa anakijua haswaa, sema hupendelea zaidi kuongea kimombo. Pengine
ndio maana mbunge wa viti maalum kutoka Zanzibar, Rukia Ahmed anahisi
mrembo huyo haijui lugha yake ya taifa.
Akiongea
bungeni leo, Bi. Rukia amesema Brigitte Alfred hafai kuiwakilisha
Tanzania kwakuwa hawezi kuzungumza Kiswahili. Mbunge huyo alienda mbali
zaidi kwa kupendekeza mashindano ya Miss Tanzania yafutwe na badala yake
yawekwe mashindano ya Sayansi kwa manufaa ya taifa.
Akijibu
kauli hiyo, Brigitte amesema: Meanwhile as our county suffers from 3rd
world problems this is what is being discussed bungeni. I would love to
meet this this woman! Asante mama,” ameandika mrembo huyo kwenye
Instagram. “All of your comments give me hope that there’s still
sensibility out here,” aliongeza.
“Mh.Rukia amekosa mada bungeni?*rollingmyeyesoutloud*,” alitweet.
“Anko in the office must be jumping for joy right now-they love to say ‘I told you so’-In Kiswahili ofcourse.”
Hata
hivyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella
Mukangara alisema serikali haiwezi kuyafuta mashindano hayo kwakuwa yana
umuhimu mkubwa kwa taifa na yamekuwa yakiitangaza nchi na shughuli za
utalii
No comments:
Post a Comment