Wekundu
wa Msimbazi simba ya jijini Dar es Salaam leo imefanikiwa kwa mara
nyinge kuzima kidomo domo, mikogo na mbwe mbwe za kila namna za watani
wao wa jadi Yanga kwa kuwafunga magoli 3-1 katika mchezo maalum wa NANI
MTANI JEMBE mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hii
leo.
katika
mchezo huo Magoli ya simba yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wake
mahiri mwenye kasi nyingi na mbinu lukuki za ufungaji Hamisi Tambwe
ambaye alipachika magoli 2 huku bao la tatu likifungwa na mchezaji
aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Mtibwa Awazi Juma huku goli la Yanga
likifungwa na Emmanuel Okwi.
Patashika ya kuwania mpira
Hali jukwaa la yanga ilikuwa si shwari sana...
Simba wao ilikuwa shangwe tu.
CHANZO : FATHER KIDEVU
Golikipa
wa Yanga,Juma Kaseja akiondosha moja ya hatari iliyokuwa inaenda
langoni kwake.Dakika 45 za kipindi cha pili ndio zimeanza hivi punde
huku mpira ukiwa ni wa kasi kwa pande zote.
Mshambuliaji
wa Timu ya Yanga,Mrisho Ngassa (17),akiwa mpiga chenga ya Mwili Beki wa
Timu ya Simba,Donald Mtosi wakati mchezo wao wa Nani Mtani Jembe
unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Hadi
hivi sasa Simba wanaongoza kwa Bao 1-0 na tayari dakika 35 za mchezo
zishakatika.Picha zote na Othman Michuzi.
Golikipa Machachari wa Timu ya Simba,Ivo Mapunda akiruka juu kudaka mpira uliokuwa unaelekea langini kwake.
Simba wakiandika Bao la Kwanza mnamo dakika ya 19 ya mchezo.
Mashabiki wa Simba
No comments:
Post a Comment