KAMATI ya
Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekutana wikiendi
iliyopita na kufikia uamuzi wa kuwapa ajira aliyekuwa katibu wa Yanga,
Selestine Mwesigwa na wa Simba, Evodius Mtawala.
Mwesigwa
atafanya kazi hiyo chini ya uangalizi kwa kipindi cha miezi sita na
endapo TFF atamudu nafasi hiyo atapewa muda zaidi, lakini kama
atashindwa basi ajira yake itasitishwa mara moja.
Wakati
Mwesigwa akiinasa ajira hiyo aliyoshindania vikali na Michael Wambura,
mwenzake wa Simba, Mtawala ameula kwenye Mkurugenzi wa Sheria na Masuala
ya Utawala ambayo ni nafasi mpya katika shirikisho hilo.
Kufuatia
uteuzi huo ni wazi Mtawala atalazimika kuachia ngazi katika nafasi yake
ya ukatibu kwenye klabu ya Simba, huku taarifa zilizoifikia Mwanaspoti
usiku wa jana Jumatatu, Mtawala ameihakikishia TFF kwamba tayari
ameshawasilisha barua yake ya kuacha kazi kwenye klabu ya Simba.
Mwesigwa na Mtawala watatangwa rasmi leo Jumanne na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
No comments:
Post a Comment