Mastaa wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline Wolper na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana na mauno waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi la Baikoko, tukio lililojiri Mwananyamala, Dar nyumbani kwa msanii mwenzao Vanitha Omary.
Wasanii hao waliwashangaza watu jinsi walivyokuwa wakijituma, kukata mauno huku Wolper akimtunza mpiga ngoma na kumkatikia kwa staili mbalimbali zikiwemo za chumbani.
Aidha, wageni waliokuwa wamealikwa eneo
hilo hawakudhani kama Wolper na Aunt wangeweza kujituma vile kama
walivyokuwa wakikata mauno hayo kwa sababu ustaa wote waliuweka pembeni
na kujiachia kwa raha zao.
Credit: Global publisher
Credit: Global publisher
No comments:
Post a Comment