30 December 2013

HIVI NDIVYO MWILI WA MWANAFUNZI WA CBE DODOMA MAREHEMU SAMWEL P. KITULA ULIVYO AGWA CHUONI HAPO JUZI

 Mnamo saa nane ( Mchana) mwili wa marehemu Samwel P. Kituliuliwasilishwa chuo cha CBE Dodoma kuagwa na wanafunzi wenzake. Baada ya hapo mwili huo unasafirishwa kuelekea mkoani kwao marehemu.
 Huu ni upande wa familia ya marehemu mbele yao kukiwa kuna sanduku lililohifadhiwa marehemu Samwel P. Kituli, aliyepatwa na umauti tarehe ya kuamukia December 26,2013 chanzo cha umauti huo ikiwa ni uvimbe wa Ini kwa mjibu wa Madaktari baada ya vipimo kubainisha tatizo hilo.
Kwaya ya Mtakatifu Cecilia kutoka CBE Roman Catholic iliyoshiriki kwenye kuaga mwili wa marehemu
 Watu wakipigwa butwaa kwa msiba huu
 Wafanyakazi wa chuo hiki nyuso zao zikiwa ni zahuzuni kwa sababu ya kipindi kigumu kilicho jitokeza, ikiwa siku ya leo tena tarehe 27/12/2013 wameondokewa na mfanya kazi Marehemu Selina Makindi hali ikiwa tete kweli.
eeeeh Mungu tusaidie
 Wadau mbali mbali waliohudhulia
Mapadree wa kiongoza misa takatifu ya marehemu Samwel
 Hawa ni viongozi kushoto ni Raisi wa (COBESO) Mhe, Remidius Emmanuelna kulia ni Mshauri wa wanafunzi

 Marehemu akinyunyiziwa maji ya baraka kwa ishara ya imani yake aliyebatizwa kwa maji ya  baraka
 Sala kwa marehemu
 Ndugu na jamaa wakiwa na majonzi mazito
 Katibu mkuu kiongozi Mhe, Dickson Msigwa kutoka serikali ya wanafunzi akisoma wasifu/historia fupi ya marehemu
 Rais wa (COBESO) Mhe, Remidius M. Emmanuel alipopata nafasi ya kusimama na kuzungumza,

 ''Ilikuwa tarehe 25/12/2013 nilipopata taarifa ya Bw. Samwel anaumwa nlienda kumuona lakini nikamkuta mke wake akaniambia amelala basi niliondoka nakutarajia kesho nirudi tena na marafiki zetu kumuona. Muda wa saa nane usiku nilipokea simu na kuambiwa Samwel amepoteza maisha.

 Samwel alikuwa nitegemeo letu kama serikali akiwa ni mshauri wetu nitamkumbuka Daima'' 

maneno ya Rais wa (COBESO).
Mshauri wa wanafunzi Mhe, L. Sikato alipopata nafasi ya kusimama ''Napongeza serikali iliyopo madarakani kufanya vyema ikiwa nina mwaka wa 7 sijawahi kuona Serikali ya wanafunzi wanatoa Fedha kwenye mfuko wao na kuchangia, hizi pongezi ziende kwa Rais wa serikali ya wanafunzi Mhe, Remidius na timu yake nzima kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa, na huu uwe mfano mzuri wa kuigwa na serikali itakayo ingia madarakani awamu nyingine tena'' 
Chuo kimejitole sanduku la marehemu na kusafirisha mwili huo. 
RAMBI RAMBI
Chuo -            200,000/=
Wafanya kazi -   72,000/=
COBESO -         50,000/=
Wanafunzi wote - 173,650/=
                  Jumla - 495650/=
 Muda wa kuaga Rais wa COBESO akitoa heshima za mwisho kwa marehemu
 Heshima za mwisho
 Safari ya kuelekea
Mshauri wa wanafunzi Mhe, L. Sikato akiwa mstari wa mblele kupeleka mwili wa marehemu  Samwel P. Kitula
Ukelewe Mkoani Mwanza

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname