23 December 2013
Barua mpya ya mfungwa Hong Kong akiwataja Wauzaji wakubwa wa Madawa ya kulevya Nchini na kutoa Onyo....!!
Waraka mwingine ulioandikwa katika lugha ya Kiswahili umechapishwa kwenye tovuti v2catholic.com... unataja majina ya Watanzania wawili kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
Waraka huo wenye ulio na saini ya aliyejiita Jumaa, akiwa jela Hon Kong, tarehe 12 Desemba 2013 ni wa kurasa mbili zilizojaa maneno ya kujuta kwa kufanya kazi hiyo
haramu, unaeleza mbinu mpya inayotumiwa na wafanyabiashara hao haramu kwa kuwatoa kafara Watanzania wanaokubali kuwa punda wa kubeba dawa hizo.
Mwishowe unatoa onyo kwa kila Mtanzania anayejiingiza katika biashara hiyo na kutoa wito wa kusambaza taarifa hii ili kuwaonya watu wengine wasithubutu kujiingiza katika biashara hiyo haramu.
Unaweza kuofya linki iliyopachikwa hapo juu kufungua na kusoma waraka huo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment