29 December 2013

ANGALIA PICHA MAUAJI YA KUTISHA KITETO


 Samahani kwa muonekano wa picha hii ila ndio hali halisi Kiteto
Mauaji yakutisha Kiteto
·      -- Wakulima wavamiwa, wachinjwa
·       -Risasi za moto zatumika
·       -Wachomewa nyumba zao
·       -RC Manyara awasili kuwapa pole
Na Mohamed Hamad
WILAYA ya Kiteto imeingia kwenye orodha ya maeneo yanayotisha kwa mauaji ya kinyama baada ya wakulima kuuawa mara kwa mara na wafugaji kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kugombea ardhi
Miongoni mwa waliouawa kinyama Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni Juma Mlagwa (49) wa Kitongoji cha Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye alivamiwa nyumbani kwake usiku na kundi la vijana wa kifugaji masai (makorianga)
Imeelezwa kuwa wakati anavamiwa zilisikika Risasi zikipigwa juu Kitongojini hapo na baada ya watu kuendelea kujificha ndani vijana hao walianza kunyinyizia nyumba zao mafuta aina ya petrol  kisha kuwasha moto
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ally Mussa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho alisema siku hiyo haitasahaulika mashani mwake kwa yaliyotokea kutokana na vitendo hivyo akisema ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu anachinjwa hadharani
“Nilichomewa Pikipiki zangu mbili pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo nguo vyakula, lakini nilichonusuri ni roho yangu ambayo hadi leo nasema najivunia uhai nilio nao”alisema Mwenyekiti huyo
Alisema chanzo cha mauaji hayo ni jamii ya kifugaji wamasai kuingiza mifugo yao kwenye shamba la mmoja wa wakulima Kitongojini hapo na baada ya kukatazwa walimpiga kisha nae kupigwa ndipo wakakusanyana kupanga uvamizi huoANGALIA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname