Dunia ina mambo, wakati wengine wanasali usiku na mchana kumwomba Mwenyezi Mungu awawezeshe kupata japo mtoto mmoja, mzazi huyu wa Brazil yeye ameona isiwe tabu, usumbufu anaoupata usiku kutoka kwa mwanaye suluhisho ni kumuweka sokoni. Mzazi huyo aliweka tangazo la kumuuza mwanaye kwenye website ya OLX katika kipengele cha watoto. Katika tangazo hilo mzazi huyo aliandika kuwa anamuuza mtoto kwa £267 ambazo ni sawa na shilingi laki 6 na kitu. Polisi wa Brazil wameanza upelelezi kufuatia tangazo hilo lililowekwa mtandaoni Jumanne katika mtandao wa OLX. Katika tangazo hilo lenye picha ya mtoto huyo mwenye umri wa miezi michache, liliandikwa 'Cries a lot and did not let me sleep and I have to work to survive.' Hata hivyo tangzao hilo lilikaa kwenye mtandao huo kwa zaidi ya masaa 12 tu kabla kampuni hiyo haijaliondoa kwenye mtandao huo kwa kukiuka vigezo na masharti ya kuweka tangazo ambalo ni ‘inappropriate content’
Source: Times Fm
No comments:
Post a Comment