08 November 2013

Utata waibuka kwenye Chupi maalum za kuzuia ubakaji nchini Uingereza

 
video-undefined-193C0E5C00000578-264_636x358
Na Damas Makangale kwa Msaada wa Mtandao
Nchini Uingereza kampuni moja ya kupambana na ubakaji wametengeza chupi maalum AR VPL ili kuzuia ubakaji wa wakinamama lakini wakosoaji wa chupi hizo wanasema zinawatia hofu wanawake kwamba vitendo vya ubakaji vimeongezeka.
Chupi aina za AR zimezinduliwa rasmi kwenye mtandao hivi karibuni (online) kusaidia kufikisha ujumbe kwa rai wa Uingereza kwa haraka sana
Chupi hizo zimekuwa zikikosolewa sana kwamba si suluhisho la ubakaji na unyanyasi wa kijinsia kwa wakinamama na wasichana wadogo kwa sababu mtu anaweza kupambana hata na kitu cha ncha kali na kuchana chupi hiyo kwenye purushani ya kutaka kumbaka.
article-0-193C57EC00000578-19_634x424
Kuundwa kwa chupi hizo kunawapa wasichana wengi faraja ya kutembea usiku, kusafiri peke yako, kwenda nje kwenye klabau za usiku.
Mradi huo ulianzishwa na chama cha watetezi wanawake wa jiji la New York (NYACK), New York
ambao wanasema kuwa walifanywa utafiti kwa miaka mitatu kabla ya kuja na aina za chupi hizo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname