Stori:Brighton Masalu na Chande Abdallah
SIKU chache baada ya Mtangazaji wa
Runinga ya ITV, Ufoo Saro kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa
baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther
Mushi, ameibuka na kula kiapo cha siri.
Ufoo ambaye alikuwa amelazwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, katika tukio la yeye kupigwa risasi,
alimpoteza mama yake mzazi aitwaye Anastazia Saro aliyedaiwa kuuawa na
marehemu Mushi aliyejiua kwa risasi.
Akizungumza na gazeti hili Ufoo alisema,
kamwe hawezi kusema kilichokuwa kikiwagombanisha yeye na marehemu Mushi
mpaka siku ya mwisho wa uhai wake.
“Siwezi kuzungumzia kabisa chanzo wala ugomvi wetu mimi na marehemu Mushi. Hiyo itakuwa siri yangu,” alisema Ufoo.
Katika mahojiano na gazeti hili,
mtangazaji huyo alipoulizwa kuhusu msimamo wake wa uhusiano baada ya
kupona kabisa alisema, hawezi kujiingiza tena kwenye mapenzi kwa sasa.
“Sitaki kabisa kusikia juu ya mapenzi,
siwezi kuliweka suala hilo akilini tena,” alijibu kwa kifupi kwa sauti
ya chini lakini yenye mkazo.
GPL
No comments:
Post a Comment