11 November 2013

Truuuuuuuuuuuuuuu laaaavu inapimwa hivii

Siku moja asubuhi mke wa Fuledi alimwambia
mmewe kuwa alihitaji fedha anunue chanuo mpya
ya kuchania nywele zake ambazo ni ndefu sana
na alipenda zikue zaidi.
Fuledi alimwambia mkewe kuwa hana hela kwani
ameshindwa hata kununua mkanda mpya na kioo
cha saa yake ya mkononi iliyoharibika.
Mke wa fuledi hakuomba zaidi ila akamwelewa
mmewe.
Fuledi akaenda kibaruani na wakati jioni anarudi
akapitia kwa fundi saa na kuiuza ile saa yake kwa
bei ya chini sana na kupitia dukani kununua

chanuo nzuri mpya.
Aliporudi akiwa amejiandaa kumpa chanuo
mkewe alishangaa kumwona mkewe kanyoa
nywele na mkononi kashika saa mpya ya kumpa
mmewe.
Kumbe na mke alikata zile nywele ndefu na kuuza
kwenye kampuni ndogo ambayo hurutubisha
nywele na kuziuza kama nywele nyingie bandia
ziuzwavyo.
Kila mtu machozi yalimtoka sio kwa uchungu ila
kwa kufurahishwa na hatua ya kila mmoja
aliyoichukua kumfanya mwenzake afurahi.
Funzo: Mapenzi sio kitu cha ajabu, kupendwa ni
kitu cha faraja ila kupendwa na kujaliwa na
unayempenda ni jambo la muhimu zaidi.
Hebu jaribu kufikiri ni mara ngapi umemfanya
afurahi yule umpendaye katika nyakati zote yaani
kwa shida na raha?

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname