14 November 2013

SIRI YAFICHUKA ...DIAMOND NA PENNY NI NDUGU..

Maajabu! Jambo zito limefichuka kuwa mastaa walio katika uhusiano wa kimapenzi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Penniel Mwingilwa ‘Penny’ ni ndugu,



Diamond kwa sasa ndiye mwanamuziki aliye matawi ya juu zaidi kuliko yeyote kwenye Bongo Fleva, akisumbua vibaya na kibao chake cha Number One wakati Penny akiingiza mkwanja kupitia utangazaji katika kituo cha Runinga ya Dar es Salaam ‘DTV’.

ISHU YABUMBURUKA!
Sosi wa karibu, ndani ya familia ya Diamond alinyetisha kwamba, Diamond na Penny ni ndugu wa damu lakini jambo hilo limefahamika hivi karibuni na hivyo wanahaha namna ya kuzima aibu hiyo.



 Penny

Kwa sharti la kutochorwa sosi huyo alisema: “Ndugu kwenye familia wanagongana. Wanajaribu kufichaficha hili jambo, lakini inashindikana. Unajua kinacholeta shida zaidi ni kwamba Diamond na Penny watakavyokuwa baada ya uamuzi kupitishwa.”
 

Alisema, pamoja na ukweli huo kugundulika bila shaka kuwa ni ndugu, bado kuna ugumu wa wapenzi hao waliozama kwenye dimbwi la mahaba kisha kuvunja amri ya sita, kuachana na kubaki wakiheshimiana kama kaka na dada.
“Tatizo ni je, Diamond atakubali kumchukulia Penny kama ndugu yake? Kama atakubali na Penny naye atakuwa tayari? Wote kwa pamoja wanaonekana kama wanapingana na jambo hilo,” alisema.
 

UNDUGU WENYEWE UKOJE?
Akieleza aina ya unasaba wa Diamond na Penny, sosi wetu huyo alisema, bibi mzaa mama wa Diamond na bibi mzaa mama wa Penny, wamezaliwa na mama mmoja.
Hapa anafafanua: “Kwa sababu hiyo sasa, unaweza kuona kuwa, wale ni sawa tu na mtu na kaka yake. Tena wako ndani ya ukoo kabisa, sema hao mabibi, kila mmoja alikuwa na baba yake, walichangia mama tu.
“Familia imejiridhisha kabisa, halafu isitoshe imeonekana kuwa, undugu wa kuchangia mama ndiyo wa uhakika zaidi kuliko wa baba ambao mtu anaweza kubambikwa hata mtoto asiye wake. Kifupi Penny na Diamond ni ndugu. Sema ndiyo hivyo historia za wazazi wao zinashangaza mpaka basi.”
Kwa mujibu wa sosi wetu, majina ya bibi hao wanaounganisha undugu ni Khadija Said Abas (bibi yake Penny) na Tatu Omar (bibi yake Diamond), wote kwa sasa wametangulia mbele ya haki.

MAMA DIAMOND ACHEKELEA
Wakati jambo hilo likileta msuguano wa kimyakimya ndani ya familia huku wengi wakitaka undugu huo uheshimiwe na uhusiano uvunjwe kabisa, imeelezwa kuwa mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ anafurahia undugu huo.
“Kinachoshangaza sasa, mama Diamond amefurahi sana na amezidisha mapenzi yake kwa Penny, ndiyo maana hataki kusikia mwanaye anakuwa na mwanamke mwingine zaidi ya Penny.
 

“Mwenyewe anasema, kwanza undugu siyo wa karibu sana hivyo haina madhara lakini pia anajua Diamond atampenda, kumheshimu na hatamnyanyasa kwa sababu ni sehemu ya damu ya familia yao,” sosi aliendelea kutiririka.
 KULE DIAMOND
Amani lilifanya juhudi za kumsaka Diamond katika simu zake zote za mkononi bila mafanikio, likahamia kwenye mitandao ya kijamii, likamnasa ambapo awali mahojiano yalikuwa na kigugumizi lakini baadaye mambo yalikuwa hivi;
AMANI: Mzee vipi, mbona hupatikani kwenye simu zako zote? Kuna jambo nataka kukuuliza bwana mkubwa.
DIAMOND: Niko Nigeria. Vipi, kuna nini tena?
AMANI: Kuna stori fulani... eti ni kweli bibi yake Penny mzaa mama na bibi yako wewe ni ndugu wa damu kwa maana wamezaliwa na mama mmoja?
DIAMOND: Yeah but wamechangia mama, kila mmoja na baba yake.
AMANI: Kwa hiyo Penny ni dada yako kiasili si ndiyo?
DIAMOND: Yap!
AMANI: Duh! Majanga... kwa hiyo unatembea na dada yako wa damu?
DIAMOND: Nilikuwa najua basi kaka?!
AMANI: Kwa hiyo sasa baada ya kugundua hivyo, unaachana naye au?
DIAMOND: Kama nilivyokuambia, niko Nigeria... halafu niko gym sasa hivi, nitakutafuta nikitoka.
AMANI: Sawa, naomba ujibu hili swali la mwisho. Tumesikia kuwa, mama yako anampenda sana Penny, ni kwa sababu amegundua kuwa una undugu naye?
DIAMOND: Ha! Ha! Ha! Nikitoka gym nitakupigia simu tuzungumze vizuri.
Diamond hakufanya hivyo. Hata alivyotafutwa baadaye kwenye mtandao huo, pia hakuonekana kuwa hewani.

PENNY MIKONONI
MWA AMANI
Penny alipopatikana juzi Jumanne, kwa njia ya simu alielezwa ilivyo ambapo alisema: “Ni kweli Diamond ni ndugu yangu wa damu. Tumegundua tukiwa tayari tumeshakuwa wapenzi.
“Hakuna jinsi tena, sanasana naona kama mapenzi yetu ndiyo yamezidi kuimarika. Nampenda sana Diamond wangu na sababu hiyo haitoshi kututenganisha maana kama ni makosa tayari yameshatokea.”

MAMA DIAMOND
Kwa upande wake mama Diamond, baada ya kusimuliwa kila kilichofika mezani mwa kutakiwa kueleza msimamo wake alijibu kwa kifupi: “Ndiyo ni kweli unayosema, lakini kwa sasa nipo huku Kariakoo (Dar), sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza. Njoo nyumbani jioni, tuzungumze vizuri.”
Diamond na Penny wamekuwa kwenye penzi lenye kasheshe nyingi kufuatia mwanamuziki huyo kuhusishwa na wanawake wengine akiwemo aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Wema Isaac Sepetu. 
-GPL

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname