Mwenyekiti
wa Simba SC, Aden Rage (katikati) akiwa na wachezaji wapya Badru Ally
(kulia) na Awadh Juma (kushoto) baada ya kusaini kuichezea Simba leo.
SIMBA SC
imesajili wachezaji wawili kwa mpigo leo hii, kiungo mchezeshaji Awadh
Juma Issa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro na Ally Badru Ally kutoka
Canal Suez ya Ligi Kuu ya Misri.
Wachezaji hao wawili wa timu ya soka ya taifa ya Zanzibar wamesaini
adhuhuri ya leo, nyumbani kwa Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden
Rage, Mtaa
wa Samora, Dar es Salaam.Walitua kwa ndege maalum na mchana wakaenda kusaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja na baada ya hapo, wakarejea kwenye kambi ya Zanzibar Heroes inayojiandaa na michuano ya CECAFA Challenge.
wa Samora, Dar es Salaam.Walitua kwa ndege maalum na mchana wakaenda kusaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja na baada ya hapo, wakarejea kwenye kambi ya Zanzibar Heroes inayojiandaa na michuano ya CECAFA Challenge.
Akizungumza baada ya kuwasajili wachezaji hao, Rage ambaye ni Mbunge
wa jimbo la Tabora Mjini (CCM), alisema kwamba usajili huo umetokana na
mapendekezo ya benchi la Ufundi."Ni wachezaji wazuri, ambao tunawajua
vizuri na tumekuwa tukiwafuatilia kwa muda mrefu na tuna imani nao sana
kwamba watakuja kuisaidia timu yetu,"alisema Rage.Kwa upande wake, Badru
alisema kwamba amefurahi sana kusaini Simba SC na anaamini nyota yake
itang'ara huko. "Simba SC ni timu kubwa, maarufu, naamini kabisa hapa
nitafanya vizuri, kikubwa tu naomba sapoti ya mashabiki wote,"alisema.
Kuhusu klabu
yake ya Misri aliyoichezea tangu mwaka 2010, Badru alisema kwamba
imemruhusu kuondoka ingawa alikuwa ana miaka miwili zaidi katika Mkataba
wake na klabu hiyo.
Juma ambaye ameichezea Mtibwa Sugar kwa miaka miwili tangu
alipojiunga nayo akitokea Taasisi ya Soka Tanzania (TSA) ambako alikuwa
pamoja na Thomas Ulimwengu alisema kwamba amefurahi kutua Msimbazi.
"Nimefurahi sana kuja Simba SC, ni ndoto zangu za muda mrefu na sasa ni wakati wa kufanya kazi tu,"alisema.
No comments:
Post a Comment