02 November 2013

"SIKUWA NAJUA MAPENZI NI NINI MPAKA NILIPOPATA MTOTO"....MWANA FA


page
Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amesema alikuwa hajui mapenzi ni kitu gani mpaka pale binti yake aliyetimizia miaka miwili hivi karibuni, Maleeka kuzaliwa.

Mwana FA amesema tangu awe na mtoto, maisha yake yamebadilika kwa kiasi kikubwa na kumfanya aishi maisha ya kujilinda zaidi kuliko zamani.
Nimekuwa very careful, I am worried, siko reckless kama nilivyokuwa. Naogopa

nina mtu ananitazama na sitaki kumwangusha. Watu wengine tumekua kidogo juu juu sana, sitaki maisha yangu ambayo mimi nimekua impitie mwanangu hata kidogo,” alisema FA.
“Amenibadilisha, nawaza, nina wasiwasi kuhusu maisha yangu ya mbele. Kiukweli maisha yangu ya kufikiri kuhusiana na maisha na vitu vingine vinavyonizunguka vimebadilika sana kwaajili ya binti.”

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname