Jarida la burudani la A-Listers limemtaja star wa movie Juliet Ibrahim kutoka Ghana kuwa ndiye mwanamke mrembo zaidi Afrika magharibi.
Juliet ambaye pia anafahamika kama Juliet Safo ni Mghana
aliyechanganyika kutoka kwa baba mwenye asili ya Lebanon pamoja na mama
mwenye asili ya Ghana na Liberia. Kati ya filamu alizowahi kucheza ni
pamoja na Crime to Christ (2005), Honor My Will (2008), “Marriage of
sorrows”(2009) na nyingine nyingi.
Mtandao wa Naija Gists wa Nigeria umeandika habari hii lakini
mwandishi ameonekana kutoridhishwa sana na kuhoji “Do you believe Juliet
Ibrahim is indeed the most beautiful woman in West Africa abi dey wan
say the most beautiful woman in Ghana?”
No comments:
Post a Comment