13 November 2013

MZEE WA MIAKA 80 AJIUA BAADA YA KUGUNDUA KUWA MKEWE ANATEMBEA NA MTOTO WAO WA MIAKA 12..

AMA kweli duniani kuna mambo! Mzee Juma Kondo (80) mkazi wa Mkuranga mkoani Pwani amejiua kwa kunywa dawa ya macho hivi karibuni kutokana na wivu wa kimapenzi.
Mke wa marehemu, Asha Ali (50) anayetuhumiwa kutembea na mwanaye wa miaka 12.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo jirani na familia hiyo, mzee Juma na mkewe, Asha Ali (50) walikuwa na mgogoro wa muda mrefu uliotokana na mambo ya mapenzi.
Mzee huyo alikuwa akimtuhumu mkewe kutembea na mtoto wao wa mwisho ambaye ana umri wa miaka 12 (jina kapuni).
“Mpaka marehemu anachukua uamuzi wa kujiua, mgogoro mkubwa kati yao ulikuwa ni kumlalamikia mkewe kutembea na mtoto wao huyo anayesoma darasa la tano,” kimesema chanzo hicho.

Waandishi wetu walizungumza na mke wa marehemu, Asha ambaye alikiri mumewe kujiua kutokana na wivu huo wa mapenzi.
“Ndani ya ndoa yetu tulikuwa na mgogoro na mume wangu alikuwa akinituhumu kutembea na mwanangu kitu ambacho hakikuwa cha kweli, binafsi siwezi kulala na mwanangu kwa sababu mimi siyo kuku.

Mtoto wa mwisho wa marehemu mwenye umri wa miaka 12 anayesoma darasa la tano anayetuhumiwa kutembea na mama'ke.
“Mara kadhaa tumeshakwenda kwa mwenyekiti kusuluhishwa lakini ilishindikana.
“Mara ya mwisho alinitaka nile kiapo kwa kushika kitabu cha dini lakini nilikataa kwa sababu siwezi kuapa kitu cha uongo na baada ya hapo tulikaa siku mbili ndipo alipokunywa hiyo dawa ya macho na kufa,” alisema mama huyo.

Pia, mke huyo alisema kuwa kuna siku mumewe alimwambia kuwa atakunywa sumu kwa sababu macho yake yalikuwa hayaoni na haoni raha ya kuishi duniani.
Mtoto wa marehemu alisema amesikitishwa na kitendo cha baba yake kumtuhumu kutembea na mama yake lakini hakuwa na la kufanya.
Kaburi la marehemu Mzee Juma Kondo (80).
“Hivi sasa naona aibu kwa kuwa mitaani nadaiwa kusababisha kifo cha baba yangu, naumia sana,” alisema mtoto huyo huku akikanusha kutembea na mama yake.
Mwenyekiti wa Mkuranga B, Abdallah Ali Kingwele amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambacho kimewaacha watu midomo wazi.
“Kabla ya kifo niliwasuluhisha lakini mzee Juma alitaka mkewe aape kama kweli hana uhusiano na mtoto wake ambapo alikataa kuapa ndipo kikao kiliishia hapo na mgogoro huo ukaendelea mpaka niliposikia amefariki dunia,” alisema mwenyekiti huyo.

Nyumbani kwa marehemu Mzee Juma Kondo.

GPL

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname