Bechi la ufundi la maafande wa jeshi la kujenga Taifa wa mkoani Pwani, Ruvu Shooting Stars limesema linahitaji kusajili wachezaji kadhaa katika dirisha dogo la usajili lililofungiliwa jana ili kuongeza nguvu kuelekea mzunguko wa kwanza.Kocha mkuu wa klabu hiyo, Charles Biniface Mkwasa `Master` , amesema kuwa kwa sasa ni mapema kusema anamsajili nani na nani, lakini kwa kwa sababu muda upo, anajaribu kutafuta wachezaji kulingana na mapungufu yake.“Kuna haja ya kuongeza, lakini bado sijaona wachezaji. Unajua timu yetuu bado tunaijenga na tuna udhaifu mwingi sana hasa sehemu ya mlinda mlango, ulinzi na ushambuliaji”. Alisema Mkwasa.
Mkwasa aliongeza kuwa walipata nafasi nyingi zaidi mzunguko wa kwanza lakini walizipoteza, walifungwa magoli mengi zaidi, na hii inamaanisha ushambuliaji ni butu, pia wanahitaji kutafuta kipa mwingine.
“Usajili unahitaji umakini mkubwa, benchi la ufundi tunahaha kutafuta wachezaji watakaotufaa zaidi ili kuwa na nguvu kubwa mzunguko wa kwanza, kikubwa mashabiki wawe na subiri kwani timu bado inajengwa”. Alisema Mkwasa.
Mkwasa alikiri ugumu wa ligi kuu kwa sasa kwani timu zimejiandaa vizuri na zinacheza soka zuri zaidi.
“Timu zina kasi kubwa, kila mtu anasaka pointi tatu muhimu, najua ugumu uliopo mbeleni, ninahitaji kuongeza nguvu zaidi na kufuta udhaifu nilionao katika kikosi changu ili kuweza kuendana na kasi ya wapinzani mara mzunguko wa pili utakapoanza”. Alisema Mkwasa.
Ruvu shooting ilianza ligi vizuri, lakini haijamaliza vizuri mzunguko wa kwanza kutfuatia kupata matokeo mabaya.
No comments:
Post a Comment